IQNA

Rais Ahmadinejad: Nowruz inatoa ujumbe wa matumaini

16:34 - March 28, 2011
Habari ID: 2098588
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ujumbe mkuu wa Nowruz ni matumaini juu ya mustakbali wenye fanaka kwa wanadamu na kuzivuka shida na tabu.
Dakta Mahmoud Ahmadinejad ameyasema hayo katika hafla rasmi ya sherehe za kimataifa za Nowruz zilizofanyika Jumamosi hapa mjini Tehran; na kuongeza kwamba endapo thamani za ishara hiyo ya uwezo wa Mwenyezi Mungu itaarifishwa kwa njia sahihi hakuna shaka yoyote kuwa itapokelewa na watu wote ulimwenguni. Sambamba na kuashiria kuwa msimu wa baridi kali kwa wanadamu unakaribia kwisha na ule wa machipuo unakaribia, Rais Ahmadinejad amesema, kudhihirihi hasa kwa Nowruz kutathibiti pale ibada ya Mungu mmoja, uadilifu na upendo vitakapotawala duniani na kutosalia athari yoyote ya madhalimu, wavamizi, dhulma na ubaguzi. Dakta Ahmadinejad amesema sikukuu ya Nowruz inasherehekewa katika nchi nyingi za Asia, Afrika, Amerika ya Latini na eneo la Balkan; na kwa niaba ya taifa la Iran ametoa mkono wa heri na baraka wa sikukuu hiyo kwa wananchi wote wa maeneo hayo. Sherehe za kimataifa za Nowruz zimehudhuriwa na viongozi wa nchi mbalimbali wakiwemo marais wa Afghanistan, Iraq, Tajikistan na Turkmanestan.
766647
captcha