Kongamano hilo litafanyika Aprili 5-6 2011. Wanaotazamiwa kushiriki ni kutoka nchi za Kiafrika, Pakistan, Malaysia, Indonesia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Kuwait, Uingereza na India.
Muhammad Zubair Mughal, Taaisi ya Al Huda ya Mfumo wa Banki za Kiislamu na Uchumi CIBE amesema ni muhimu kuimarisha mfumo wa kifedha na banki za Kiislamu barani Afrika. Aidha amesema kuna haja ya kustawisha benki za biashara na taasisi ndogo ndogo za fedha (MFIs) ili kusaidia katika kuendoa umasikini na kuimarisha miundombinu ya serikali.
Tayari benki za Kiislamu au huduma za Kiislamu katika benki za kawaida zinastawi kwa kasi huko Kenya, Tanzania, Afrika Kusini, Misri, Sudan na Nigeria. Aidha serikali za Ghana, Uganda, Ivory Coast na Somalia zinafanya juhudi za kuanzisha banki za Kiislamu.
766710