Vyama hivyo pia vimewataka Wabahrain washiriki katika maombolezo ya mashahidi hao hapo siku ya Jumamosi. Vyama hivyo pamoja na jumuiya za kijamii za Bahrain pia zimewataka Wabahrain kuzuri makaburi ya mashahidi hao waliopoteza maisha katika maandamano yao halali ya kulalamikia hali mbaya ya kisiasa ya nchi hiyo kila siku ya Alkhamisi. Wakati huohuo, Joe Stork, Mkuu wa Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch anayesimamia masuala ya haki za binadamu katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika amelaani vikali kitendo cha watawala wa Bahrain cha kutumia askari wa kigeni katika kukandamiza na kuwaua ovyo wananchi wanaoandamana kwa amani kwa ajili ya kufuatilia matakwa yao. Stork ambaye hivi karibuni aliutembelea mji mkuu wa nchi hiyo Manama amebainisha wasiwasi wake mkubwa kutokana na hatua za watawala wa nchi hiyo za kutumia mabavu dhidi ya raia wa kawaida wasio na hatia. 767287