IQNA

Masomo maalumu ya mahafidh wa Qur'ani yafanyika Bahrain

11:36 - March 31, 2011
Habari ID: 2099292
Idara Kuu ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Imarati siku ya Jumanne iliandaa masomo maalumu kwa ajili ya Mahafidh wa Qur'ani Tukufu huko katika Msikiti wa Muhammad bin Zayed katika mji mkuu Abu Dhabi.
Kwa mujibu wa gazeti la Ittihad linalochapishwa nchini Imarati, masomo hayo yaliyowashirikisha mahafidh 60 kutoka taasisi mbalimbali za Qur'ani na vituo vya kidini vya Imarati yalitoa mafunzo maalumu ya kuinua viwango vyao vya kielimu na hifdhi ya Qur'ani Tukufu. Kuwafahamisha washiriki thamani na sifa za jamii pamoja na kukidhiwa mahitaji yake na hasa yanayohusiana na masuala ya Qur'ani ni baadhi ya malengo ya kuandaliwa masomo hayo. 767238
captcha