IQNA

Mashindano ya Qurani ya wanajeshi wa Iran kufanyika

13:30 - April 03, 2011
Habari ID: 2099806
Mashindano ya Kitaifa ya Qurani kwa ajili ya Vikosi vya Kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatafanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mei 17-18.
Mashindano hayo yatajjumuisha viwango kama vile qiraa , hifdi, tarjumi na tafsiri ya Qurani Tukufu na vile vile Adhana na Hadithi. Mashindano ha Hadithi yameongezwa kwa lengo la kuwahimiza washiriki kufahamu kwa kina mafundisho ya Ahlul Bayt AS sambamba na Qurani Tukufu.
Mashindano hayo ya siku mbili yatamalizika kwa sherehe za kuwatunuku zawadi washindi. Washiriki wa mashindano hayo watajumuisha wale watakaofuzu katika mashindano ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC , Jeshi la Polisi na Wizara ya Ulinzi.
764034
captcha