Waandamanaji wametaka kuuzuliwa kwa viongozi hao kwa tuhuma kwamba wamekuwa wakitumia vibaya taasisi na mashirika ya kidini ya Misri na hasa Chuo Kikuu cha al-Azhar dhidi ya maslahi ya kitaifa ya nchi hiyo. Wamesema kuwa viongozi hao waovu waliwakandamiza wananchi wakati wa kufanyika maandamano dhidi ya mfumo wa Mubarak na kutaka taasisi zote za kidini za nchi hiyo zisafishwe kutokana na viongozi kama hao wanaotumia vibaya dini kwa malsahi yao binafsi. Takwa hilo limetolewa siku moja tu baada ya wanachama wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya al-Azhar kutangaza uungaji mkono wao kwa Ahmad Tayyib kama msimamizi wa Chuo cha al-Azhar. 767999