Terry Jones, kasisi wa uongo na mwovu wa Marekani ambaye ametekeleza tishio lake la kuchoma moto Qur'ani Tukufu na hivyo kuamsha hasira ya Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia, si tu kwamba hajaona haya kuhusiana na kitendo chake hicho cha dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu, bali ametangaza kuongoza maandamano yaliyo dhidi ya Uislamu tarehe 22 ya mwezi huu wa Aprili mbele ya msikiti mmoja huko katika jimbo la Michigan.
Akizungumza katika tukio hilo la kusikitisha huko katika kanisa la Dove World Outreach Center katika mji wa Gainesville jimboni Florida, Terry Jones amedai kuwa kitendo chake hicho kiovu cha kuchoma moto Qur'ani ni kuimarisha mwamko wa watu kuhusiana na kile alichokitaja kuwa mambo ya kufurutu ada katika Uislamu! Hii ni katika hali ambayo kitendo hicho kimewakera sana Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia na Waislamu wa nchi kama vile Pakistan na Afghanistan wamefanya maandamano makubwa ya kutaka kufikishwa kasisis huyo mwovu mbele ya vyombo vya sheria, lakini watawala wa Marekani wamekuwa wakikwepa kufanya hivyo kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza na hivyo kushajiisha kuendelea kwa vitendo vya dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu nchini humo. 767847