IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qurani ya Kuwait kuanza

0:36 - April 04, 2011
Habari ID: 2099989
Mashindano ya Kimataifa ya Qurani ya Kuwait yamepangwa kuanza Jumatano Aprili 13 katika mji mkuu wa nchi hiyo Kuwait City.
Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Kuwait la Ar Ray, mashindano hayo yatakuwa na viwango vya kuhifadhi Qurani nzima, hifdhi inayojumuisha aina saba za kusoma na qiraa.
Mashindano hayo yameandaliwa na Wizara ya Aqqaf na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait. Jopo la majaji katika mashindano hayo linajumuisha wataalamu bingwa wa Qurani wenye uzoefu.
Ili kuhakikisha mashindano yanabakia katika kiwango cha juu, jopo la majaji lina uwezo wa kubadilisha sheria za mashindano.
Serikali ya Kuwati imetenga zawadi maalumu za kifedha kwa watakaoibuka washindi katika mashindano hayo.
767915
captcha