IQNA

16:53 - April 04, 2011
Habari ID: 2100523

Harakati za Kiislamu za Misri kuunda 'Muungano wa Kiislamu'

Harakati na makundi ya Kiislamu ya Misri yameazimia kubuni muungano mmoja wa Kiislamu.

Viongozi wa harakati na makundi hayo ya Kiislamu walikutana hivi karibuni na kujadili masuala muhimu yatakayopelekea kubuniwa kwa muungano huo muhimu wa kisiasa uliosimama juu ya misingi ya mafundisho ya kidini. Wanazuoni na wahadhiri mashuhuri wa vyuo vikuu ni miongoni mwa wanachama wa kamati kuu ya muungano huo wa baadaye wa Kiislamu. 768488
captcha