IQNA

Kesi ya mtengenezaji filamu ya Fitna kuendelea hivi karibuni

16:52 - April 04, 2011
Habari ID: 2100524
Jaji Judge Marcel van Oosten anayeendesha kesi ya Geert Wlders, mbunge mwenye misimamo ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi amesema kuwa kesi hiyo itaaanza tena tarehe 13 Aprili huko mjini Amsterdam.
Mbunge huyo amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuchochea hisia za kibaguzi na chuki dhidi ya Waislamu nchini humo. Mbunge huyo pia amekuwa akipigania kupigwa marufuku uuzwaji Qur'ani Tukufu nchini Uholanzi pamoja na kuutuhumu Uislamu kuwa ni dini ya ufashisti. Awali mbunge huyo alikuwa amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na kutozwa faini ya euro 7600 kuhusiana na vitendo vyake vya kuchochea ubaguzi na chuki dhidi ya Waislamu. Katika filamu yake ya dharau dhidi ya matukufu ya kidini aliyoipa jina la Fitna, Wilders aliutuhumu Uislamu kuwa chanzo cha ugaidi duniani jambo lililowakasirisha mno Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia. Licha ya malalamiko na maandamano makubwa yaliyofanywa ulimwenguni na Waislamu kupinga jambo hilo, lakini mbunge huyo muovu angali anafanya jitihada za kutengeneza filamu nyingine kama hiyo dhidi ya matukufu ya Kiislamu. Katika filamu yake ya kwanza Wilders aliutaja Uislamu kuwa adui wa kwanza wa uhuru wa mwanadamu na kuwatuhumu Waislamu kuwa makatili. 768393
captcha