Misikiti mingi iliyochomwa moto inapatikana katika mtaa wa Hamad. Utawala huo pia umekuwa ukiwafuta kazi kiholela na kutowalipa mishahara watu walioshiriki katika maandamano ya hivi karibuni nchini humo wakitaka kufanyika marekebisho ya kisiasa katika muundo wa utawala huo. Wanafunzi na wanachuo walioshiriki katika maandamano hayo pia wamefukuzwa mashuleni na vyuoni. Wanazuoni wa Bahrain wanasema kuwa watawala wa nchi hiyo hata wamekuwa wakizuia watu waliojeruhiwa katika machafuko ya hivi karibuni kupata matibabu katika mahospitali ya nchi hiyo na kuwazuia madaktari kutoka nchi nyingine ambao wameomba kuingia nchini humo kwa lengo la kuwatibu majeruhi hao bila malipo. Utawala wa Manama umeanzisha wimbi kubwa la ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika nchi hiyo na hata umekuwa ukiwatia mbaroni wanawake wajawazito na walio na umri mkubwa bila kujali lolote wala kuzingatia misingi ya utu katika kufanya hivyo. 768401