IQNA

Maandalizi ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qurani Iran yaanza

10:39 - April 05, 2011
Habari ID: 2100643
Kikao cha kupanga mikakati ya Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qurani kimefanyika Aprili nne mjini Tehran.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Seyyed Mohammad Husseini na naibu wake katika masuala ya Qurani Hujjatul Islam Hamid Mohammadi pamoja na maafisa wengine husika.
Mkutano huo ulijadili njia za kufanikisha maonyesho hayo. Aidha waliochangia katika maonyesho ya 18 ya Qurani walienziwa.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qurani hufanyika kila mwaka katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Maonyesho hayo hujumuisha athari mbali mbali za kielimu , kisanaa na kiteknolojia za Qurani Tukufu. Aghalabu ya nchi za Kiislamu hushiriki katika maonyesho hayo.
768553
captcha