IQNA

Harakati ya Jihad ni Msingi wa Maendeleo

10:38 - April 05, 2011
Habari ID: 2100831
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuyakurubisha Madhehebu ya Kiislamu Ayatullah Mohammad Ali Taskhiri amesema ustawi ndio msingi wa uadilifu wa kijamii na msingi wa uadilifu ni harakati ya Jihadi.
Akizungumza na IQNA kuhusu hatua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kislamu kuutaja mwaka huu wa Kiirani wa Hijria Shamsia (Kuanzia Machi 21 2011-Machi 21 2012) kuwa mwaka wa Jihadi ya Kiuchumi, Ayatullah Taskhiri ameitaja Jihad kuwa kujitahidi kwa kiwango cha juu ili kufukia lengo.
"Hali ilivyohivi sasa inaibua dharura ya kufanya sekta zote za maisha yetu kuwa ni Jihadi", amesema. "Katika uga wa uchumi vile vile, harakati ya Jihadi inapaswa kuzingatiwa zaidi".
Akifafanua kuwa neno Jihad linamaanisha kuwa neno Jihad linamaanisha kutafuta njia za kufikia lengo, amesema kuwa neno hilo pia linamaanisha kupambana na maadui. Amesema maadui wanajaribu kuzuia maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
768364
captcha