IQNA DIRISHA KUELEKEA ULIMWENGU WA KIMAANAWI
Shirika la Habari la Quran la Iran IQNA ndio la kwanza, la pekee ambalo linashughulikia kwa njia maalumu habari za Quran katika ulimwengu wa Kiislamu. Juhudi zetu daima zimekuwa ni kusambaza habari na ripoti za Iran na ulimwengu mzima kwa ujumla kuhusu masuala yanayohusiana na Quran Tukufu pamoja na habari kisiasa, kitamaduni, kisanaa, kijamii vijana na watoto pamoja na kuzitathmini kwa mtazamo wa Quran Tukufu.
HISTORIA:
Shirika la Habari la Qur’an la Iran IQNA lilianzishwa tarehe 15 Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1424 Hijria sawa na 11 Novemba 2003. Sherehe za uzinduzi wa shirika hili zilihudhuriwa na Hujjatul Islam wa Muslimin Sayyid Muhammad Khatami (Rais wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran”, Bw. Masjid Jam’e (Waziri wa wakati huo wa Utamaduni na Muongozi wa Kiislamu), wakuu wa kitengo cha Jihad katika vyuo vikuu pamoja na wanazuoni na wataalamu wa Qur’an Tukufu Wafanyakazi wa shirika la habari la IQNA wanajitahidi kufanya kazi zao kwa kumtegmea Mwenyezi Mungu na miongozo ya Qur’an Tukufu na kwa kufuata mkondo wa Imam Khomeini (MA), Kiongozi Muadhamu na mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Malengo:
Malengo muhimu yanayozingatiwa na Shirika la Habari la Quran la Iran IQNA ni kama ifuatavyo:
1. Kuhimiza utamaduni aali na wa kumjengwa mwanadamu wa Qur’an Tukufu kati ya watu wa tabaka mbali mbali katika jamii.
2. Kupasha haraka habari kamili kuhusu harakati na shughuli zinazohusiana na Qur’an Tukufu nchini Iran na duniani kote.
3. Kuzalisha na kusambaza habari zinazoakisi masuala ya Qura’n Tukufu katika medani mbali mbali.
4. Kuhimiza uzingatiwaji wa mitazamo ya Qur’an Tukufu katika masuala na kadhia mbali mbali za kisayansi, kisanaa, kutamaduni, kisiasa, kifasihi, kijamii n.k
5. Kuakisi mazingira ya Quran Tukufu yanayotawala katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyinginezo za Kiislamu duniani.
6. Kuinua kiwango cha kuifahamu Qur’an Tukufu miongoni mwa matabaka mbali mbali ya jamii
7. Kubadilishana uzoefu na vigezo vilivyofanikiwa katika miradi ya Qur’an Tukufu nchini Iran na katika uga wa kimataifa.
8. Kuanzisha mikakati ya kitamaduni na kifikra katika masuala mbali mbali kwa kuzingatia Qur’an Tukufu kama mhimili mkuu.
SHUGHULI MUHIMU:
Shughuli za IQNA zinaweza kufafanuliwa ifuatavyo:
1. Kuandika habari na kutayarisha mahijiano kila siku katika vipengee mbali mbli vya habari.
2. Kuandaa vikao vya uchambuzi wa habari vinavyowashirikisha wataalmu, weledi wa mambo, wasomi na maafisa mbali mbali husika.
3. Kutayarisha na kuchapisha jarida la kila wiki mbili la habari la IQNA lijulikanalo kama “Rayhe” (Harufu Nzuri)
4. Kuakisi kikamilifu, ipasavyo na kwa njia maalumu matukio na harakati maalumu za Qur’an katika vyombo vya habari vya ndani na kimataifa.