Watafiti waliofanya uchunguzi huo wanasema kuwa matokeo ya uchunguzi wao utasaidia kutambuliwa wahanga hasa wa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na kuwasilisha njia bora za kuhudumiwa wahanga hao. Wamesema uchunguzi huo umefanyika kwa ajili ya kuweka wazi matatizo yanayowakabili wanawake wa Kiislamu wanaovaa hijabu raia wa Uingereza na kuwasilisha njia za kuwalinda kutokana na vitendo vya chuki na ubaguzi. Wamesema vitendo vingi vya chuki hiyo hutekelezwa katika maeneo ya umma na kutoripotiwa kwa polisi na hivyo kuzuia haki za wahanga kufuatiliwa mahakamani. Wanawake wa Kiislamu wanaovaa hijabu walioshirikishwa katika uchungzi na utafiti huo ni raia wa Uingereza walio na asili ya nchi za Kiislamu za mabara ya Asia na Afrika. Watu wolio na hamu ya kushiriki katika kikao cha kutangazwa matokeo hayo katika chuo kilichotajwa wako huru kufanya hivyo. 769542