Kwa mujibu wa shirika la habari la Malaysia Bernama, kikao hicho kimechunguza na kujadili njia za kuimarisha mfumo wa sheria wa nchi hiyo kwa msingi wa sheria za Kiislamu. Datuk Jamil Khair bin Baharom, Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Malaysia na wawakilishi kadhaa wa serikali pamoja na wawakilishi wa Shirika la Ustawi wa Kiislamu la Malaysia wameshiriki katika kikao hicho ambapo wamejadili masuala mengi yanayohusiana na sheria za Kiislamu ikiwemo historia na changamoto zinazozuia kutekelezwa vyema kwa sheria za Kiislamu nchini humo. 769884