IQNA

Kukumbukwa siku ya kuuawa shahidi Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir Uholanzi

12:07 - April 07, 2011
Habari ID: 2101962
Maadhimisho maalumu yamepangwa kufanyika nchini Uholanzi kwa ajili ya kukumbuka kuwadia mwaka wa 31 wa kuuawa shahidi mar'ja na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Muhammad Baqir Swadr (MA) pamoja na dada yake Bintul Huda.
Makumbusho hayo yameandaliwa na Taasisi ya al-Kauthar ya hukohuko Uholanzi. Miaka 31 iliyopita Sayyid Muhammad Baqir Swadr akiwa pamoja na dada yake waliuawa shahidi kinyama tarehe 8 Aprili mwaka 1980 huko Iraq na askari katili wa utawala wa kidikteta wa Saddam Hussein uliong'olewa madarakani hivi karibuni. Maadhimisho hayo yamepangwa kufanyika hapo kesho Ijumaa. 769815
captcha