Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qurani kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kiislamu Senegal.
Mashindano hayo yatajumuisha tajweed na hifdhi ya Qurani Tukufu na yataendelea kwa siku nne.
Kati ya watakaohudhuria mashindano hayo ni Rais Abdoulaye Wade wa Senegal, Abdullah Al Mohsen Al Turki Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Duniani na Abdullah Ben Ali Besfer Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qurani.
Mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kuwahimiza vijana kujifunza kusoma na kuhifadhi Qurani Tukufu na kuwaelimisha zaidi kuhusu ufahamu wa Qurani Tukufu.
771537