IQNA

Kikao cha Waarabu chachunguza hali ya Gaza

16:34 - April 11, 2011
Habari ID: 2104205
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ilifanya kikao cha dharura hapo siku ya Jumapili kwa ajili ya kuchunguza mashambulio ya utawala haramu wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
Kikao hicho ambacho kimeitishwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina kimechunguza mashambulio ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi na waliozingirwa na utawala huo huko Gaza pamoja na kujadili njia za kusimamisha mashambulio hayo ya kinyama. Akizungumzia mashambulio hayo, Hamad bin Hilli, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa mashambulio hayo ni katika mfululizo wa mashambulio ambayo yamekuwa yakifanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina wasio na hatia kwa kipindi cha miongo sita iliyopita na kwamba yamesadifiana na wakati wa kufanyika mashambulio mengine ya kinyama kama hayo dhidi ya Wapalestina huko katika kijiji cha Dir Yasin mwaka 1947. Katika kipindi cha siku mbili zilizopita, utawala haramu wa Israel umekuwa ukishambulia vituo vya tiba, mahospitali, shule na nyumba za Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambapo watu wapatao 17 wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa. 771717
captcha