Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani yafanyika Mauritania
Mashindano ya kitaifa ya hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani Tukufu yalianza siku ya Jumapili katika msikiti wa Ijumaa wa mji mkuu wa Mauritania Nouakchott.
Washindani 256 wanashiriki katika mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa ajili ya kuwachagua washindi watakaoiwakilisha nchi hiyo katika mashindano ya Qur'ani katika nchi mbalimbai za Kiarabu na Kiislamu. Tabia na maadili bora ya washiriki pia yatazingatiwa katika kuwachagua wawakilishi hao. 772390