IQNA

Kozi za ‘Kuhubiri Uislamu’ kufanyika Tanzania

12:26 - April 12, 2011
Habari ID: 2104614
Kozi maalumu za ‘Kuhubiri Uislamu’ maalumu kwa mubalighina au wahubiri na waliosilimu zitafanyika Dar-es-Salaam Tanzania kwa himya ya Kitengo cha Tablighi cha Wakala wa Waislamu Afrika kwa ushirikiano na Kamati ya Kutoa Misaada ya Kuwait.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Afrika Mashariki, kozi hii itajumuisha mafunzo kuhusu Seerah ya Mtume Mtukufu SAW, dini ya Kiislamu na kuishi kwa maelewano watu wa dini mbali mbali.
Aidha washiriki wamepewa mafunzo kuhusu utumizi wa hekima katika kuhubiri na namna ya kutekeleza ibada na maamurisho ya kidini.
772293
captcha