IQNA

Shirika la Misaada la Kiislamu Kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afrika Sudan

12:39 - April 12, 2011
1
Habari ID: 2104628
Mkataba wa ushirikiano umetiwa saini baina ya Shirika la Kimataifa la Kiislamu la Misaada na Chuo Kikuu Kimataifa cha Afrika cha Sudan kwa lengo la kuhimiza harakati za utoaji misaada.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Sudan, makubaliano haya yametiwa sainia na Adnan bin Khalil Basha Katibu Mkuu wa ya Shirika la Kimataifa la Kiislamu la Misaada na Hassan Maki Mohammad Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika Cha Sudan. Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Jeddah Saudi Arabia.
Taasisi hizo mbili zitashirikiana katika kuhimiza utoaji misaada na malezi.
Pande mbili zitatumia uzoefu na wataalamu katika kutekeleza shughuli za utoaji misaada kote duniani.
771482
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 2
Mwinshekhe
0
0
Assalamualaikum,,,mwangalie jicho lenu la huruma kwa nchi za Afrika hasa hasa Tanzania kuna changamoto kubwa kwa walimu wa dini wa elimu ya msingi (awali) walimu wengi wana hali mbaya za kimaisha kwa mfano mimi ni mwalimu wa dini nina wanafunzi zaidi ya khamsini ninaowafundisha sehemu ya madarasa vitabu hatuna pia hata mishahara ya walimu kwa kukimu sehemu ya maisha yao ili kuwezesha kurithisha vyema elimu hii tunaomba mliangalie hili kwa jicho la huruma
captcha