IQNA

Mapenzi ya Ahlul Beit (as) kuinganishi cha pamoja cha Iran na Misri

17:43 - April 13, 2011
Habari ID: 2105479
Ahmad al-Ghamrawi Mkuu wa Jumuiya ya Urafiki wa Iran na Misri amesema kuwa mapenzi kwa Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) ni kiunganishi cha pamoja cha watu wa nchi mbili hizi za Kiislamu.
Akizungumza huko Cairo katika kikao cha kuchunguza uhusianao wa baadaye wa Iran na Misri, al-Ghamrawi amesema kuwa licha ya kuwa wanchi wengi wa Misri ni wafuasi wa madhehebu ya Sunni lakini ni wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) na hivyo jambo hilo kuwa kiunganishi muhimu cha watu wa nchi hiyo na wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Huku akisema kuwa madola ya Magharibi yanapinga kuboreshwa kwa uhusiano wa Misri na Iran kwa kisingizio kuwa kunahatarisha maslahi yao, al-Ghamrawi amesema kuwa nchi hizo zimekuwa zikifanya njama kubwa za kuzusha fitna na mgawanyiko kati ya Waislamu wa madhebu ya Shia na Suni. Akizungumza katika kikao hicho, Mujtaba Imani, msimamizi wa ofisi ya kulinda maslahi ya Iran nchini Misri amesema kuwa wasomi na wanafikra wa Kiislamu wanapasa kutafuta njia za kuimarisha uhusiano wa mataifa mawili haya ya Kiislamu. Ameashiria matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Nabil alArabi Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri kwamba kuna haja ya kuhuishwa uhusiano wa kidiplomasia wa Iran na Misri Imani amesema kuwa uhusiano huo unapaswa kucunguzwa katika mtazamo wa matukio mapya katika Mashariki ya Kati na hasa kufuatia mapinduzi ya hivi karibuni nchini Misri. Amesema nchi mbili hizi zina uwezo wa kuboresha uhusiano wao kwa maslahi ya pande mbili. 773863
captcha