IQNA

Nchi 28 zashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Senegal

17:43 - April 13, 2011
Habari ID: 2105480
Mashindano ya kimataifa ya hifdhi na usamoji Qura'ni yanaendelea nchini Senegal kwa kuhudhuriwa na nchi 28. Mashindano hayo yaliyoanza siku ya Jumatatu yanawashirikisha vijana wa umri wa kati ya miaka 12 hadi 20.
Akizungumzia mashindano hayo Muhammad Sayyid Ba, Katibu Mkuu wa Shirika la Ustawi na Mafunzo ya Kiislamu la Senegal amesema kwamba Senegal imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kutokana na nafasi yake nzuri katika mafunzo ya Qur'ani. Amesema marefa wa mashindano hayo wamechaguliwa kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu. Mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika. Mashindano hayo yanatazamiwa kumalizika hapo kesho Alkhamisi. 773594
captcha