IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yaanza Kuwait

17:44 - April 13, 2011
Habari ID: 2105482
Awamu ya pili ya mashindano ya kimataifa ya hifdhi, tajwidi na usomaji Qur'ani yameanza leo Jumatano nchini Kuwait kwa kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 50.
Mashindano hayo yameandaliwa na Idara ya Masuala ya Qur'ani inayofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait. Marefa wa mashindano hayo ni wasomaji mashuhuri wa Qur'ani kutoka nchi za Kiislamu zikiwemo wa Misri, Saudi Arabia, Syria, Morocco na Kuwait. Mashindano hayo yatamalizika rasmi hapo siku ya Jumanne tarehe 19 Aprili. 773600
captcha