Orodha hii ni ya mashirika yanayouza bidhaa na huduma halali. Habari za kuanzishwa Orodha ya Halali ya SAMI zimetolewa na Thomson Reuters na Taasisi ya Ideal Ratings nchini Malaysia wiki jana. Kuanzishwa orodha hiyo kunaashiria ustawi wa sekt aya fedha ya Kiislamu na viwanda vya bidhaa na huduma halali katika nchi hiyo.
Ideal Ratings ni shirika lenye makao yake San Francisco nchini Marekani na hukagua huduma za kifedha za Kiislamu kote duniani.
Orodha ya Halali ya SAMI inajumuisha mashirika 200 katika nchi za Kiislamu ambayo kwa pamoja yana mtaji wa zaidi ya dola bilioni moja.
Kati ya mashirika hayo 200, 95 yako Malaysia yakiwa na mtaji wa dola bilioni 53 na mashirika yaliyosali ni kutoka Saudi Arabia , Uturuki, Indonesia na Nigeria.
773939