IQNA

Kozi ya kielimu ya wanawake Waislamu Nigeria

8:54 - April 14, 2011
Habari ID: 2105595
Kozi ya kielimu maalumu kwa wanawake Waislamu inafanyika katika Husseiniya (ukumbi wa hafla za kidini) ya Baqiyatullah AS huko Zaria kaskazini mwa Nigeria.
Washiriki katika kozi hiyo ambao aghalabu ni wanawake wa Kishia watapata mafunzo kuhusu masuala ya kieleimu na kidini kama vile fiqhi, misingi ya Kiislamu na hukumu za kisheria za wanazuoni wa Kiislamu kwa msingi wa mafundisho ya Qurani.
Washiriki pia watajadili matatizo katika maeneo yao na kujaribu kuyatafutia suluhu.
Baada ya kozi hiyo kutakuwa na mtihani wa kutathmini uwezo wa wanawake hao kukabiliana na changamoto mbali mbali maishani.
Wanawake Waislamu kutoka maeneo mbali mbali ya Nigeria huhudhuria kozi hiyo ambayo hufanyika baada ya kila miezi mitatu. Kozi hiyo iliyoanza Aprili 12 inamalizika Aprili 14.
773709

captcha