IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Uholanzi

12:12 - April 16, 2011
Habari ID: 2106283
Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya mwaka huu wa 2011 ambayo yameandaliwa na jumuiya pamoja na taasisi tofauti za Kiislamu za nchini Uholanzi yanaendelea katika miji tofauti ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, mashindano hayo yanafanyika baada ya kufanikiwa mashindano mengine kama hayo ambayo yalifanyika nchini humo mwaka uliopita wa 2010. Mashindano hayo yanawajumuisha watu walio na umri tofauti watoto kwa wazee, wanaume kwa wanawake na wavulana kwa wasichana. Sheria za usomaji Qurani zitapaswa kuheshimiwa na kulindwa na washiriki wote wa mashindano hayo. Sherehe za kuhitimisha mashindano hayo zinatazamiwa kufanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Amsterdam hapo siku ya Jumatatu tarehe 18 Aprili. 774470
captcha