IQNA

Semina ya 'Mohammad SAW; Rehma kwa Walimwengu' yafanyika Uturuki

13:27 - April 16, 2011
Habari ID: 2106401
Semina yenye anuani ya 'Mohammad SAW; Rehma kwa Walimwengu' imefanyika mjini Istanbul na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Uturuki Rajab Tayeb Erdogan
Kemal Kılıçdaroğlu kiongozi wa chama cha RPP na Mehmet Görmez Mkuu wa Shirika la Masuala ya Kidini la Uturuki pia walishiriki katika semina hiyo.
Erdogan alitoa hotuba kuhusu fadhila za kimaadili za Mtume SAW pamoja na hadithi zake.
Kwa mnasaba wa Wiki ya Umoja na Maulidi ya Mtume SAW inayofanyika kati ya Aprili 14 -20 nchini Uturuki, Shirika la Masuala ya Kidini limezindua tovuti yenye anuani ya www.merhamet.org
774481
captcha