Katika kitengo cha hifdh, washiriki walio na umri wa chini ya miaka 16 watashindana katika hatua tatu za kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 15 na juzuu 5 za kitabu hicho kitakatifu. Katika kitengo cha usomaji, washindani watachuana katika hatua mbili za kusoma Qur'ani nzima huku wakichunga kanuni na sheria za tajwidi kwa walio na umri wa chini ya miaka 11 na usomaji wa Qur'ani nzima kwa wanaoanza usomaji wa Qur'ani walio na umri wa chini ya miaka 7. Mashindano hayo ya kitaifa huandaliwa kila mwaka na Muungano wa Kiislamu wa Marekani Kaskazini kwa madhumuni ya kuwashajiisha watoto na vijana wajishughulishe zaidi na usomaji pamoja na hifdhi ya Qur'ani Tukufu. 775722