Kikao hicho kimeandaliwa na Kituo cha Utafiti wa Kiislamu na Ukristo kinachofungamana na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yusuf cha mjini Beirut. Kwa mujibu wa tovuti ya lebanonfiles kikao hicho kimefanyika katika fremu ya ratiba ya chuo hicho ya kuimarisha uhusiano wa Waislamu na Wakristo. Lengo jingine la kikao hicho ni kuimarisha ushirikiano wa wataalamu na watafiti wa masuala ya Kiislamu na Kikristo katika kunyanyua kiwango cha elimu ili kushuhghulikia vyema suala la kuimarishwa uhusiano wa pande mbili hizi na kukabiliana na njama za maadui wao wa pamoja. 777118