Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la Peninsula, wazungumzaji wa kikao hicho walisisitiza juu ya kuzingatiwa mafundisho ya Qur'ani kwa lengo la kumuongoza mwanadamu kwenye njia nyoofu humu duniani na kumdhaminia saada huko Akhera. Wamesema kuwa kitabu hicho kitakatifu kinapaswa kuzingatiwa kwa kina kwa sababu ndicho kinachamdhaminia mwanadamu maisha mema humu duniani na huko Akhera. Wazungumzaji ambao walikuwa raia kutoka Qatar na India walisisitiza umuhimu wa kuzingatia Waislamu mafundisho ya kitabu hicho ili yaweze kuwanufaisha katika maisha yao ya mtu binafsi na ya kijamii. Zawadi pia zilitolewa kwa washindi wa mashindano ya Qur'ani yaliyoandaliwa na Kituo cha Marekebisho cha India kilicho na makao makuu yake mjini Doha na ambacho ndicho kilichoandaa kikao hicho. 777280