IQNA

Msikiti wakosewa heshima huko Ubelgiji

11:14 - April 20, 2011
Habari ID: 2108952
Siku ya Jumanne watu wasiojulikana katika mji wa Charleroi huko Ubelgiji wameukosea heshima msikiti mmoja unaoendelea kujengwa katika mji huo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP watu hao waliingia katika msikiti huo unaomilikiwa na Jumuiya ya Waislamu ya Tuba hapo siku ya Jumanne usiku na kuandika kwenye kuta zake maandishi ya matusi na dharau dhidi ya Uislamu kukiwemo kumkosea heshima Mtume Mtukufu (saw). Katika hatua nyingine ya chuki na dharau dhidi ya Uislamu watu hao wasiojulikana walichora kwenye msikiti huo alama ya misalanba iliyovyunjwa pembeni ya maandishi hayo ya kumkosea heshima Mtume Mtukufu (saw). Baada ya kufahamishwa jambo hilo polisi ya mji huo ilifika mahala hapo mara moja na kuanzisha uchunguzi ili kuwatia nguvuni wahalifu waliohusika na kitendo hicho. Wakati huohuo Haratakati inayopinga ubaguzi wa rangi ya Ubelgiji imelaani kitendo hicho cha ubaguzi wa rangi na kutaka wahusika hao wa kukosewa heshima misikiti wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo. 777538
captcha