Jamii ya Waislamu wapatao milioni mbili mjini Moscow, mji mkuu wa Russia, ambayo ina misikiti minne tu imetaka misikiti iongezwe mjini humo.
Kwa mujibu wa tovui ya cnb licha ya kuwa Moscow ni mji ulio na idadi kubwa zaidi ya Waislamu kati ya miji ya Ulaya, lakini ina misikiti mine tu jambo linalofanya maelfu ya Waislamu walazimike kuswali kwenye maeneo ya wazi na mabarabara yanayoizunguka misikiti hiyo. Akilalamikia jambo hilo, Eldor Ayat ad-Deen, imam wa moja ya misikiti ya Moscow amesema iwapo hali hiyo itaendelea ni wazi kuwa katika siku zijazo Waislamu watalazimika kutekelezea ibada zao kwenye makanisa. Amesema viongozi wengi wa Russia wanaufahamu vibaya Uislamu na ndio maana wakawa wanapinga ujenzi wa misikiti nchini humo kwa kisingizio cha ugaidi. Kutokana na kutokuwepo takwimu za kuaminika kuhusiana na idadi ya Waislamu wanaoishi mjini Moscow, serikali ya nchi hiyo inasema kuwa idadi hiyo kidogo inazidi milioni moja ilhali, jumuiya za Waislamu zinasema kuwa ni watu milioni mbili. Melfu ya Waislamu waliokuwa wakiishi katika nchi za Muungano wa Russia, walihamia katika mji mkuu Moscow, mara tu baada ya kusambaratika kwa muungano huo mwaka 1991. 777648