IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani yaanza Paris

13:00 - April 23, 2011
Habari ID: 2110338
Muungano wa Jumuiya za Kiislamu Ulaya umeandaa mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Mashindano hayo yamaenza Ijumaa Aprili 22 pembizoni mwa Mkutano wa 28 wa Waislamu Ufaransa.
Mahafidh wa Qurani kutoka miji mbali mbali ya Ufaransa yanashiriki katika mashindano hayo ya siku mbili.
Aidha pembizoni mwa mkutano huo wa Waislamu Ufaransa kutakuwa na maonyesho ya sanaa za Kiislamu, utamaduni, uadilifu wa kijamii, uchumi katika Uislamu, vyakula halali, hali ya Uislamu Ufaransa na Ulaya.
Kauli mbiu ya mkutano huo utakaomalizika Aprili 25 imetajwa kuwa ni 'Kukabiliana Waislamu na Changamoto za Sasa.
Muungano wa Jumuiya za Kiislamu Ulaya (Union des organisations islamiques de France) ulibuniwa mwaka 1983. Muungano huo unawakilisha jumuiya mbali mbali za Kiislamu Ufaransa ni ni kitengo cha Ufaransa cha Muungano wa Jumuiya za Kiislamu Ulaya.
778553

captcha