Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zimefanyika katika Msikiti Mkuu wa Sultan Said bin Taimur mjini Muscat.
Mashindano hayo yanafanyika katika ngazi tano tofauti za hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na tajwidi, hifdhi ya juzuu 24 pamoja na tajwidi, hifdhi ya juzuu 18, hifdhi ya juzuu 12 na hifdhi ya juzuu 6.
Katika mashindano hayo pia kunatumiwa teknolojia ya kisasa ya kufanya tathmini ya viwango cha usomaji Qur'ani.
Malengo ya mashindano ya sasa wa Qur'ani ya Oman yametajwa kuwa ni pamoja na kuhamasisha usomaji Qur'ani na kutekeleza mafundisho yake, kulea kizazi cha wasomaji mahiri wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutayarisha washiriki wenye uwezo mkubwa wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani. 779621