IQNA

Wanaharakati wa haki za binadamu walaani uvamizi dhidi ya mahospitali

14:10 - April 25, 2011
Habari ID: 2111609
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yasiyo ya kiserikali ya Bahrain yamelaani vikali hatua ya kinyama ya watawala wa kifalme wa nchi hiyo ya kuvamia mahospitali na kuwatia nguvuni madaktari na majeruhi wanaotibiwa kwenye mahospitali hayo.
Katika upande wa pili, Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International lenye makao makuu mjini London, Uingereza limeyataka madola ya Magharibi yanayoshirikiana na utawala wa kifalme wa Bahrain kuulazimisha utawala huo usimamishe mara moja vitendo hivyo visivyo vya kibinadamu.
Mashirika ya kutetea haki za kiraia yanayopinga utawala dhalimu wa Bahrain yametangaza kwamba mamia ya wafanyakazi wa nchi hiyo wamefutwa kazi kwenye idara za serikali kutokana na misimamo yao dhidi ya utawala huo.
Mashirika hayo yamezitaka nchi za Magharibi zinazouunga mkono utawala wa Manama kutokana na maslahi yao binafsi ya kistratejia kuvunja kimya chao kuhusiana na dhulma pamoja na jinai zinazofanywa na utawala huo dhidi ya Wabahrain wasio na hatia. Mashirika hayo yanasema kuwa nchi hizo ambazo hivi karibuni zimekuwa zikipiga makelele mengi kuhusiana na kuvunjwa haki za binadamu katika nchi za Misri, Libya na Tunisia hivi sasa zimenyamaza kimya mbele ya mauaji na jinai zinazofanywa na watawala wa Bahrain dhidi ya raia wa nchi hiyo ili kulinda maslahi yao katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.
Shirika la madaktari wasio la mpaka lenye makao makuu mjini Paris, Ufaransa limesema kuwa utawala wa Bahrain umebadili mahospitali ya nchi hiyo kuwa maeneo ya kutisha na kutia hofu kwa sababu madaktari, wahudumu na majeruhi wanaofikishwa kwenye mahospitali hayo wanakamatwa na kuteswa na askari usalama wa nchi hiyo kwa ushirikiano wa askari wa kigeni wa Saudi Arabia. 780022
captcha