IQNA

Ufaransa mwenyeji wa kikao cha 'Uislamu katika Jamii ya Ulaya'

13:41 - April 25, 2011
Habari ID: 2111611
Kikao cha tatu cha kimataifa cha 'Uislamu katika Jamii ya Ulaya' kinachodhaminiwa na shirika la Ufaransa la Ustaarabu wa Kiislamu kimepangwa kufanyika hapo siku ya Jumatano katika mji wa Lyon.
Kikao hicho ambacho kitafanyika kwa ushirikiano wa msikiti mkuu wa Lyon kimepangiwa kujadili nafasi ya Uislamu barani Ulaya, vikwazo vinavyowakabili Waislamu katika utekelezaji bora wa majukumu yao ya kidini na pia suala la manufaa ya Uislamu kwa raia wengine wa Ulaya.
Shakhsia na wasomi wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu na zisizo za Kiislamu wamealikwa kuzungumza katika kikao hicho. 780258
captcha