Washiriki zaidi ya 200 wanashindana katika Olimpiadi ya kwanza ya Qur'ani itakayowashirikisha wanafunzi, wahadhiri na wafanyakazi wa chuo hicho.
Baada ya kushiriki katika mtihani ulioandikwa, washiriki wanajitayarisha kwa ajili ya mtihani wa qiraa, hifdhi, tarjuma na tafsiri.
Kwa mujibu wa afisa wa habari katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Mafunzo ya Qur'ani Tukufu Mahdi Qobadi, mashindano hayo yatafanyika katika Wilaya ya Meybod mkoani Yazd.
Qari mashuhuri wa kimataifa Ali Asghari Shoaie ni kati ya wataalamu wa Qur'ani watakaoshiriki. Ustadh Shoaei ni Mkurugenzi wa Kituo cha Qur'ani katika chuo hicho.
Chuo Kikuu cha Sayansi za Qur'ani kina matawi 14 kote nchini Iran. Chuo hicho kinasimamiwa na Shirika la Waqfu la Iran na hutoa mafunzo yanayuhusiana na nyanja mbalimbali za Qur'ani Tukufu.
780431