Kwa mujibu wa gazeti la The Times of Pakistan kumbi 50 za Kiislamu au Husseiniya pia zimebomolewa katika hujuma hiyo ya pamoja ya vikosi vya Saudia na Bahrain. Kati ya misikiti iliyobomolewa ni ile iliyo katika maeneo ya Karzakan, Salmabad, Bu Quwah, na A’ali. Baadhi ya ripoti zinasema idadi ya misikiti iliyobomolewa imepindukia 30.
Wabahrain walianza maandamano Februari 14 wakitaka utawala wa kifalme wa Aal Khalifa unaopata uungaji mkono mkubwa wa Marekan,i uondoke madarakani.
Katika hujuma hiyo dhidi ya misikiti Bahrain misahafu iliyokuwemo ndani imeteketezwa kwa moto na vikosi hivyo vya tawala za kifalme za Aal Saud na Aal Khalifa.
Ili kulalamikia jinai hiyo ya kuchomwa moto Qur'ani Tukufu na kuvunjwa misikiti wananchi waumini wa Bahrain siku ya Ijumaa iliyopita waliitangaza kuwa ‘Ijumaa ya Qur'ani Tukufu.'
aandamanaji nchini Bahrain wamesema hawatalegeza misimamo yao ya kutaka kuuondoa madarakani utawala wa Aal Khalifa ambao pia unapata uungaji mkono wa Marekani. Aidha vyama vya upinzani vimeanzisha kampeni ya kimataifa chini ya anwani ya ‘Misikiti Yetu, Maisha Yetu' ili kulaani sera za kuvunja misikiti za utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain.
Maandamano makubwa yamefanyika pia nchini Iran na katika nchi kadhaa duniani kulaani hatua ya wanajeshi wa Bahrain na Saudia ya kuchoma moto Qur'ani Tukufu.
779622