IQNA

Duru ya pili ya mashindano ya Qur'ani yamalizika Saudia

17:19 - April 26, 2011
Habari ID: 2112581
Sherehe za kuhitimishwa duru ya pili ya mashindano ya kitaifa ya shule za hifdhi ya Qur'ani zinafanyika leo Jumanne huko katika mji wa Jeddah, Saudi Arabia.
Sherehe hizo zimeandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani ambayo inafungamana na Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu na kusimamiwa na Mash'al bin Majid, Gavana wa Jeddah. Katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo ambayo yamefanyika kabla ya sherehe za leo, washindi 30 walioshinda katika hatua ya mwanzo wamechuana katika makundi matatu ya shule za sekondari, madarasa ya juu ya shule za msingi na vilevile wanafunzi wa madarasa ya chini ya shule hizo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kubainishwa nafasi muhimu ya shule za hifdhi ya Qur'ani katika jamii, kushajiishwa wanafunzi waimarishe hifdhi ya Qur'ani, kuarifishwa wanafunzi bora wa masomo ya Qur'ani pamoja na kuimarishwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani na Wizara ya Elimu na Malezi ya Saudia ni miongoni mwa malengo ya kuandaliwa mashindano hayo. 781105
captcha