IQNA

Mji wa Jakarta washurutisha masomo ya Qur’ani

13:32 - April 28, 2011
Habari ID: 2113428
Mji wa Jakarta nchini Indonesia umetoa sharti la kuwataka wanafunzi wote Waislamu wajifunze kusoma na kuandika aya za Qur'ani Tukufu.
Gavana wa Jakarta Fauzi Bowo amesema sawa na miji mingine yenye Waislamu wengi nchini Indonesia, mji huo utatekeleza sheria za kuwataka wanafunzi wote wajifunze Qur’ani Tukufu.
Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa kampeni ya kusoma Qur’ani katika Msikiti wa At-Tin mashariki mwa Jakarta, gavana huyo amesema atatia saini sheria hiyo hivi karibuni.
Indonesia yenye idadi ya watu milioni 238 ndio nchi yenye idadi ya Waislamu wengi zaidi duniani.
782379
captcha