IQNA

Hifadhi ya data ya mashahidi wa Lebanon kuzinduliwa

13:36 - April 28, 2011
Habari ID: 2113528
Hifadhi ya data au benki ya data ya mashahidi wa mapambano ya Kiislamu nchini Lebanon itazinduliwa hivi karibuni na Jumuiya ya Uhuishaji wa Turathi za Mapambano ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Intiqad linalochapishwa huko Lebanon, hifadhi hiyo itatumia teknolojia ya kisasa kabisa katika kutoa hudumu kwa watu wanaotaka kunufaika na maelezo ya maisha pamoja na habari nyingine muhimu zinazohusiana na mashahidi wa mapambano ya Kiislamu.
Picha, mahojiano na jamaa, marafiki pamoja na jamaa wa mashahidi na vilevile bidhaa na vifaa walivyotumia mashahidi kabla ya kuuawa kwao ni miongoni mwa mambo yatakayokusanywa katika hifadhi hiyo ya data.
Jumuiya iliyotajwa ya Lebanon tayari ina kituo kipya cha kuhifadhia athari za mashahidi hao katika Kituo cha Imam Kadhim (as) kilichoko katika mtaa wa Madhwi, kwa lengo la kuhuisha na kulinda heshima ya mashahidi wa mapambano hayo. 782422
captcha