Katika ujumbe wake maalumu, Ayatullahil Udhma Lotfollah Safi-Golpaygani ametoa wito kwa vyuo vya kidini na wasomi wa Kiislamu kote duniani kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu nchini Bahrain.
"Kwa nini duru za Kiislamu na viongozi wa kidini na kiutamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu wamenyamaza kimya pasina kukosoa vitendo vya kubomolewa misikiti na kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Bahrain?", amehoji mwanazuoni huyo.
Ayatullah Golpaygani ametoa wito wa kutumwa timu nchini Bahrain kwa lengo la kusitisha vitendo vya kubomolewa misikiti na kuvunjiwa heshima Qur'ani ambavyo vinatekelezwa na vikosi vya Bahrain vikishirikiana na wanajeshi vamizi wa Saudia.
"Vikosi (vya Saudia na Bahrain) vimeteketeza moto Misahafu na kubomoa karibu misikiti 30", amesema kuhusu vitendo hivyo vya kusikitisha.
Wabahrain walianza maandamano Februari 14 wakitaka utawala wa kifalme wa Aal Khalifa unaopata uungaji mkono mkubwa wa Marekani uondoke madarakani.
Katika hujuma hiyo dhidi ya misikiti Bahrain Misahafu iliyokuwemo ndani imeteketezwa kwa moto na vikosi hivyo vya tawala za kifalme za Aal Saud na Aal Khalifa.
Waandamanaji nchini Bahrain wamesema hawatalegeza misimamo yao ya kutaka kuuondoa madarakani utawala wa Aal Khalifa ambao pia unapata uungaji mkono wa Marekani.
782625