Khatibu wa sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema kuwa, wananchi wa eneo hili ndio watakaoibuka washindi katika mapambano yao ya Kiislamu dhidi ya madikteta.
Huku akiashiria kusimama kidete wananchi wa eneo la Mashariki ya Kati dhidi ya madikteta, Ayatullah Seyyid Ahmad Khatami amesema kuwa, kwa kuzingatia tajiriba ya kihistoria ya karne nyingi, wananchi wa eneo hili wataushinda mfumo wa kibeberu. Ayatullah Khatami aidha amebainisha kuwa hii leo nchi ya Bahrain imebadilishwa kuwa jela kubwa kwa uungaji mkono wa Marekani na utawala wa kifalme wa Aal Saudi kwa utawala wa Aal Khalifa na kuongeza kuwa, tawala hizo mbili za kifalme za Kiarabu kila zinavyoendelea kufanya jinai ndivyo zinavyopiga hatua kuelekea kwenye maangamizi.
Khatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran aidha amekosoa kimya cha Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na baadhi ya maulamaa wa Kiislamu mkabala na mauaji na ukandamizwaji unaofanywa dhidi ya wananchi wa eneo hili na kuzitaka taasisi hizo ziache kukaa kimya na kuwatetea wananchi wanaokandamizwa.
783056