Tarjumi hiyo ijulikanayo kama 'The Quran: An English Translation' imechapishwa na Taasisi ya Mareknai ya Historia ya Kiislamu na Utamaduni yenye makao yake California.
Dr. Nazeer amesema tarjumi hiyo inalenga kuwasilisha ujumbe wa Qur'ani kwa Wamarekani kwa lugha sahali hasa kwa kuzingatia kuwa Wamagharibi wamepotoshwa sana kuhusu Uislamu.
Tarjumi hiyo imezinduliwa na Maulana Riyazur Rahman Imamu wa Msikiti wa Jamia wa Bangalore.
Dr. Nazeer alizaliwa mjini Tumkur karibu na Bangalore na alijiuna na Shirika la Marekani la Anga za Mbali NASA mwaka 1973 ambako alihusika na mradi wa kutengeneza gari la Landrover kuenda mwezini. Baadaye alikuwa mhandisi mkuu wa maabara ya kutegeneza teleskopu aina ya Hubble.
Dr. Nazeer ameandika vitabu kadhaa kuhusu dini, sayansi na filosofia na vilevile Ensaiklopidia ya Historia ya Kiislamu inayopatikana katika www.historyofislam.com yenye kurasa 9,000.
783283