Kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa la Le Figaro Muhammad Musawi, mkuu wa baraza hilo ametoa taarifa akibainisha wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na tuhuma hizo zinazotolewa dhidi ya jamii ya Waislamu nchini Ufaransa na kuongeza kuwa ameshangazwa mno na tuhuma hizo ambazo zinadai kuwa Msikiti Mkuu wa Lyon unatumiwa kuwapa mafunzo ya ugaidi baadhi ya watu walio na misimamo ya kupindukia mipaka. Amesema tuhuma hizo ni za kipumbavu na zisizo na msingi na kuwa bila shaka zimechochewa na viongozi wa Marekani. Amesema tuhuma hizo hazikubaliki kabisa kwa kutilia maanani kwamba wawakilishi wa Marekani nchini Ufaransa wamekuwa wakiutembelea msikiti huo mara kwa mara na kufahamishwa vyema shughuli zake.
Akizungumzia suala hilo Jean-François Carenco, Gavana wa Jimbo la Rhone pia ametoa taarifa akipinga tuhuma hizo za Wamarekani dhidi ya Msikiti wa Lyobn na kuongeza kuwa hazina msingi wowote.
Katika nyaraka zilizotolewa hivi karibuni, wawakilishi wa Congress ya Marekani wamedai kuwa Msikiti wa Lyon nchini Ufaransa ni kituo muhimu cha kupewa mafunzo ya ugaidi Waislamu wenye misimamo ya kupindukia mipaka barani Ulaya, tuhuma ambazo zimeamsha hasira ya Waislamu wa nchi hiyo. 783028