Kutoa taarifa za kulaani jinai za Aal Saud na Aal Khalifa nchini Bahrain hakutawasaidia Waislamu wa nchi hiyo ambao wanatetea haki zao za kisheria, amesema Abdul Rauf Shayeb kiongozi wa Harakati ya Uhuru ya Bahrain.
Amesema jinai zinazotekelezwa na Aal Khalifa na Aal Saud dhidi ya watu wa Bahrain ni mauaji ya halaiki dhidi ya watu wanaotetea haki zao katika maandamano ya amani.
Ameongeza kuwa, 'kuvunjia heshima misikiti na vituo vya Kiislamu na kutusi sharia za Mtume SAW ni mambo ambayo yameumiza nyoyo za Waislamu'.
Amesema nchi za Kiislamu na Kiarabu zina majukumu kuhusu Bahrain na kuongeza kuwa nchi za Magharibi zinapaswa kulaumiwa kutokana na jinai zinazojiri Bahrain.
781812