IQNA

Kituo cha Kiislamu cha 'Udugu' chafunguliwa Ufaransa

14:09 - May 01, 2011
Habari ID: 2115138
Kituo cha Kiislamu cha 'Udugu' kilifunguliwa jana Jumamosi huko katika mji wa Limay nchini Ufaransa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Leparisien mamia ya Waislamu, maafisa wa serikali na wanazuoni wa mji huo na miji mingine jirani walihudhuria ufunguzi wa kituo hicho. Ujenzi wa Kituo cha Kiislamu na Msikitu wa Udugu uliodhaminiwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Ibn Sina umechukua muda wa miaka mitatu. Hata hivyo ramani ya ujenzi wa kituo hicho ilikabidhiwa meya wa mji huo mwaka 1997.
Pierre Bedier meya wa zamani wa Limay ambaye pia ni mbunge wa chama tawala cha UMP ni miongoni mwa watu waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa kituo hicho.
Kituo hicho ambacho kinajumuisha msikiti, ukumbi wa mikutano na madarasa ya kufundishia Qur'ani Tukufu kina uwezo wa kupokea watu 800. 784051
captcha