IQNA

Chama cha kisiasa cha Ikhwan Muslimeen chaundwa Misri

14:06 - May 01, 2011
Habari ID: 2115140
Harakati ya Ikhwanul Muslimeen ya Misri imebuni chama cha kisiasa kwa jina la Chama cha Uhuru na Uadilifu kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao.
Kufuatia kuongezeka mwamko wa Kiislamu nchini Misri na mapinduzi yaliyopelekea kung'olewa madarakani dikteta Hosni Mubarak, harakati ya Ikhwanul Muslimeen imepata nguvu mpya katika matukio ya kisiasa ya nchi hiyo na imelazimika kuunda chama cha kisiasa hapo jana tarehe 30 Aprili kwa lengo la kushiriki katika uchaguzi ujao.
Ikhwanul Muslimeen imetangaza kuwa chama hicho kitakachopigania masuala na haki za kiraia kitakuwa huru na kwamba hakitajishughulisha na masuala ya kidini wala Kiislamu ya wanachama wa harakati hiyo. Hatua hiyo imechukuliwa ili kukwepa mibano na vikwazo vya kisheria vilivyobainishwa katika katiba ya Misri dhidi ya vyama vya kidini. Hiyo ndio maana chama hicho kipya kikatangazwa kuwa ni cha kujitegemea wala hakifungamani na sera za harakati ya Ikhwanul Muslimeen.
Uchaguzi mkuu wa bunge la Misri umepangwa kufanyika Septemba ijayo. 784106
captcha